Wednesday, November 27, 2013

Babu Seya, mwanae kufia jela, rufaa yagonga mwamba



JANA Rufaa ya wanamuziki wawili Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanae Papii Nguza iligonga mwamba baada ya rufaa hiyo kutupiliwa mbali kwa kuoenekana hakuna sababu ya kurudia kesi hiyo

Kufuatia maamuzi hayo yaliyotolewa na Mahakama ya Rufani Tanzania, imedhihirisha wanamuziki hao watafia jela baada ya juhudi za kujinasua kugonga mwamba.


Mara baada ya maamuzi hayo kutolewa na mahakama hiyo, vilio ,huzuni vilitawala kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wanamuziki hao 


Umati wa watu ulifurika jana katika viunga vya mahakama hiyo kufuatialia mapitio ya rufaa hiyo na iliyokuwa ikiendeshwa na majaji watatu wa mahakama hiyo ambapo waliongozwa na Mwenyekiti wao Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati 


Hivyo mara baada ya mapitio hayo mahakama ilitamka maombi ya Babu Seya na mwanae yalitupiliwa mbali na kusema wataendelea na kifungo hicho kwakuwa hukumu yake ya awali ilikuwa sahihi.


Wamesema hoja zilizotolewa na wanamuziki hao hazina nguvu na wameonekana bado wana hatia ya makosa yao matano kati ya makosa 23 yaliyokuwa yakiwakabili likiwemo la kulawiti wanafunzi wa shule ya msingi.


Kulingana na sheria zinavyosema hatua ya jana ya kugonga mwamba kwa rufaa hiyo ni ya mwisho kabisa hakuna jinsi ya wanamuziki hao kuachiwa huru 
Sheria inasema hata Rais japo ni mkuu wan chi hana mamlaka ya kuingilia kulingana na maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo hata kama wakiwaona huruma

Awali Februari 11, mwaka 2010 mahakama hiyo iliwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya ambao waliunganishwa katika kesi hiyo baada ya kuonekana hakuna ushahidi wa kutosha ulioonyesha kwamba wana hatia katika makosa hayo


Juni, 2004, Mahakama ya Kisutu iliwahukumu Babu Seya na wanawe kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha

No comments:

Post a Comment